Microsoft word - maagizo ya kujiunga na shule.docx

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA RUVU
SHERIA ZA SHULE


1.0 UTANGULIZI
Sheria au kanuni ni utaratibu unaowabana watu kutende mambo mema katika jumuiya. Ni taratibu zinazowezesha watu wanaotoka katika mazingira mbalimbali kuwa na mwelekeo unaofanana na hivyo kuwezesha utengamano katika jamii. Shule ni sehemu ya jamii yenye lengo la kutoa elimu kurithisha matendo mema ya jamii husika. Kwa kuzingatia ukweli kuwa wanafunzi hutoka katika jamii mbalimbali ni lazima kuwepo na mtazamo wa pamoja unaolenga katika kufanikisha utoaji wa elimu bora. Ilivyo sheria ni utaratibu unaowezesha kuwepo malezi bora kwa vijana. Kila mwanafunzi ni lazima afanye juhudi kuzifahamu na kuzingatia sheria za shule kwani kutozifahamu hakitakuwa kisingizio cha kutochukuliwa hatua husika za kinidhamu endapo utakiuka. Tafadhali zingatia yafuatayo:-
2.0 SARE RASMI YA SHULE
i) Sketi ya kijani na blauzi nyeupe yenye mikono mifupi ii) Viatu vyeusi vya ngozi 3.0 USAFI
3.1 Mwanafunzi anatakiwa kuwa msafi muda wote
3.2 Asuke nyewele kuanzia mistari mitano hadi tisa au anyoe ziwe fupi
3.3 Asifuge kucha ndefu na haruhusiwi kupaka kucha rangi
3.4 Usafi uzingatiwe katika maeneneo yote ya shule pamoja na madarasani, mabwenini, vyooni, na
bwaloni
3.5 Ni marufuku kutumia dawa zinazogeuza rangi ya mwili.
3.6 Mwanafunzi asivae mapambo kama vile bangili, vipili, shanga, hereni n.k.

4.0 UTUNZAJI WA MALI YA SHULE/UMMA
4.1 Mwanafunzi azingatie matumizi sahihi ya mali ya umma (kitanda, viti, madawati, vitabu, na vifaa vya
usafi.)
4.2 Mwanafunzi aepuke tabia ya kuchora au kuandika kwenye kuta za majengo na sehemu nyingine. Ni
marufuku kuandika kwenye mbao za matangazo au ubao wa darasani.
4.3 Ni marufuku kuburuza meza, dawati, au kiti. Vifaa hivi vinyanyuliwe inapobidi kusogezwa
4.4. Maabara zisitumiwe kama hakuna mwalimu.
4.5. Ni marufuku kuwasha moto wa aina yoyote katika eneo lolote. Mishumaa na mafuta ya taa au petrol
haviruhusiwi kueletwa shuleni.
5.0 MABWENI
5.1 Ni marufuku wanafunzi wawili kukaa au kulala kitanda kimoja.
5.2 Ni marufuku kupeleka au kula chakula cha aina yoyote bwenini
5.3 Ni marufuku kubaki bwenini wakati wa masomo au wa kazi za nje.
6.0 BWALO LA CHAKULA
6.1 Chakula kiliwendani ya bwalo,
6.2 Vifaa vya bwaloni visihamishwe bila idhini ya mwalimu.
6.3 Ni marufuku wanafunzi kuingia jikoni bila idhini ya mwalimu wa zamu.
7.0 TABIA NA MWENENDO MZURI
7.1 Mara zote yule anayejiheshimu ataheshimiwa na wenzake.
7.2. Onyesha heshima pale walimu au mtu aliyekuzidi umri anapopita karibu nawe kwa kusimama.
7.3 Sio adabu njema kuongea na mwalimu au mtu aliyekuzidi umri umeshika mifukoni
7.4 Makosa ya kufukuzishwa shule mwanafunzi ni wizi, kunywa pombe, kuvuta bangi, sigara au aina
yoyote ya kilevi, kupigana, utoro, uasherati, mimba, kuolewa, kutoa mimba makosa ya jinai, kudharau
bendera ya taifa, kugoma, kuchochea na kuongoza au kuvuruga amani na usalama wa watu na kukataa
adhabu.
7.5 Ni marurufuku kutumia lugha ya matusi/isiyofaa
7.6 Ni marufuku kuwa na urafiki wa kimapenzi na mtu yeyote shuleni ama nje ya shule.
7.7 Wageni kamwe wasikaribishwe bwenini. Wageni wote watapokelewa na mwalimu wa zamu au ofisi ya
Mkuu wa shule.
7.8 Ni marufuku kwa mwanafunzi kuwa na simu ya mkononi (mobile phone) radio na vitu vyenye thamani
kubwa shuleni.

8.0 UTARATIBU WA KUTOKA NJE YA SHULE
Mwanafunzi akisharipoti shuleni hana ruhusa ya kutoka bila ruhusa rasmi
8.1 Iwapo mwanafunzi atakuwa na shida yoyote yenye uzito wa kutosha, kama ataweza kurudi siku hiyo
hiyo ataomba ruhusa kwa mwalimu wa zamu na kupewa pass ya kurudi siku hiyo.
8.2 Kama mwanafunzi atahitaji ruhusa ya kulala nje ya shule, ruhusa hiyo itaombewa kibali kwa mkuu wa
shule. Mzazi au mlezi wa mwanafunzi husika atasaini pass aliyopewa na mwanafunzi ili kuthibitisha kuwa
alikuwa kwake.
8.3 Mwanafunzi yeyote atakayeenda nje ya shule bila ruhusa atarudishwa nyumbani kumleta mzazi wake
na siyo mlezi wa muda.
8.4 Endapo mwanafunzi atatoka nje ya shule kwa kibali anatakiwa kurudi shuleni kabla ya saa 10.00 jioni.

9.0 KUITIKA KENGELE
9.1Mara tu kengele igongwapo wanafunzi wote wanatakiwa kwenda mahali husika mara moja.
9.2 Patokeapo jambo la dharura kengele ya dharura itagongwa kuashiria, hivyo ni lazima wanafunzi wote
wakimbie kuelekea eneo la (paredi) kujipanga. Kutokuwepo kwa wakati ni kosa la kumsababishia
mwanafunzi kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kumrudisha nyumbani kumleta mzazi
ili ashirikishwe tabia ya mwanae.

10.0 MAHUDHURIO

a) Mahudhurio ya darasani au kazi za mikono ni ya lazima kwa kila mwanafunzi. b) Vipindi vya usiku (preparation) ni vya lazima kwa wanafunzi wote.
11.0. MENGINEYO
11.1 Wanafunzi wote watalala saa nne (4) usiku na huo ndio muda wa kuzima taa. Mwanafunzi
atakayekutwa nje ya bweni lake baada ya muda huo atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
11.2 Ni marufuku kwa mwanafunzi kupiga kelele zisizo na sababu, kwa mfano kumwita mtu aliye mbali kwa
sauti ya juu .
11.3 Wanafunzi wote wazingatie kuwa nyumba za wafanyakazi ni nje ya shule hivyo watatembelea huko
kwa idhini ya mwalimu.
M.V. Minde
MKUU WA SHULE
HALMASHAURI YA WILAYA KIBAHA 
SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA RUVU 
MLANDIZI 
                                                                                                                                                                         22/03/2011 
SIMU: 0754 814541/ 0752 945599/ 0713 477619  Ndugu  :……………………………………………………….  YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE 
1.0 UTANGULIZI 
Ninayo furaha kukuarifu kuwa umechaguliwa kuendelea na Elimu ya sekondari kidato cha tano katika shule hii. 
Unapaswa kufika shuleni tarehe 11/04/2011 kabla ya saa 11.00  jioni. Shule ipo tarafa ya Mlandizi Wilaya ya Kibaha 
Mkoa wa Pwani kilometa 77 kutoka Dar es salaam kando ya barabara kuu iendayo Morogoro. 
2.0  MAMBO MUHIMU YA  KUZINGATIA 
2.1.ADA NA MICHANGO YA SHULE 
2.1.1 Ada ya shule ni Tshs. 70,000/= kwa mwaka au Tshs .35,000/= kwa muhula . 
2.1.2 Michango 
 
Tahadhari 
Fedha za ada na michango zilipwe kwenye akaunti Na. 2121200100 NMB Kibaha. Jina la akaunti hiyo ni Ruvu Girls 
High School

2.1.3 Fedha kwa ajili ya:‐ 
 
Kitambulsho 
Fedha hizi (Tshs 16,000/=) zilipwe kwenye akaunti Na. 2122300003 NMB Kibaha. Jina la akaunti Ruvu Girls High 
School 
2.2 Shule haipokei fedha taslimu. 
Fedha zote zilipwe kupitia Benki ya NMB TAWI LOLOTE, kwa kutumia namba za   
akaunti husika na stakabadhi za malipo (Bank pay inslips) zenye jina la mwanafunzi ziletwe shuleni siku ya kuripoti. 
2.3 Uje na nakala ya hati halisi  ya uraia au cheti cha kuzaliwa 
2.4 Uje na Nakala ya hati yako ya matokeo ya kidato cha NNE 
2.5 Uje na barua hii pamoja na nakala ya sheria za shule, fomu ya uchunguzi wa afya iliyojazwa na daktari na fomu 
ya kukubali kujiunga na shule. FOMU ZOTE NA MAELEKEZO MENGINE UTAYAPATA KATIKA TOVUTI YA SHULE  
. Fungua icon ya ADMISSION. 
2.6 
Nguo za nyumbani haziruhusiwi mwanafunzi atavaa sare za shule muda wote awapo shuleni. 
2.7 Kila mzazi /mlezi anapaswa kugharamia usafiri wa mwanae kuja shuleni na kurudi nyumbani wakati wa likizo na 
kumpa fedha za kutosha kwa ajili ya matumizi. Ruhusa za kufuata fedha za matumizi hazitolewi. 
3.0 SARE YA SHULE 
3.1.Sketi nne  (4) za heshima zenye marinda ( rangi ya kijani (dark green) mbili (2) na bluu  (dark blue)mbili (2) 3.2 Masharti meupe mikono mifupi mawili 3.3 Soksi nyeupe jozi mbili 3.4 Viatu vya kufunika vyeusi vya ngozi jozi 2 3.5 T‐shirt rangi ya kijivu isiyo na maandishi 2 3,6 Truck suit au jeans isiyobana kwa ajili ya maandalizi ya kujisomea usiku 3.7 Kwa waumini wa dini ya Kiislam sketi iwe ndefu ,shati nyeupe mikono mirefu na hijapu nyeupe wakati wa maspomo na majumba meusi kwa ajili ya kazi za nje.  4.0 MAHITAJI MENGINE 
4.1 Bunda (ream) za karatasi mbili (2)  A‐4 KWA MWAKA 
4.2  Bukta rangi ya bluu moja 
4.3 Raba za michezo pea moja 
4.4 Shuka 4 rangi ya pinki 
4.5 Mto na foronya 
4.6 Ndoo 1, dumu 1 kubwa, na dumu 1 dogo kwa ajili ya kutunzia maji ya kunywa 
4.7 Kijiko,sahani, bakuli na kikombe kwa ajili ya chai 
4.8 Tochi ya betri kwa tahadhali ya umeme ukukatika (ISIWE YA KUCHAJI) 
4.9 Madaftari makubwa (counter books) angalau kumi(10) au zaidi 
4.10 Scientific calculator kwa wanafunzi wa sayansi 
4.11Kitambulisho cha bima ya afya kama anacho 
4.12 Uwe na sh.3000/= kwa ajili ya kununulia tai 
 
5.0 VIFAA VYA USAFI 
5.1 Fagio la ndani lenye mpini mrefu (soft broom) 1 
5.2 Fagio gumu la chooni lenye mpini (hard broom) 1 
5.3Chelewa ndefu ya nje ( fagio la wima) 1 
5.4 Squeezer moja (mpira wa kukaushia maji) 1 
5.5 Fagio refu la buibui 1 
5.6 Brashi ya kusugulia choo yenye mpini mfupi 1 
 
 
TAFADHALI SOMA KWA MAKINI MAAGIZO HAYA NA KUYATELEKEZA KIKAMILIFU
KARIBU SANA 
ELIMU NI UKOMBOZI 
M. V. Minde  
(MKUU WA SHULE 
KIBAHA DISTRICT COUNCIL 
RUVU GIRLS HIGH SCHOOL
REQUEST FOR MEDICAL EXAMINATION
From the Headmistress Ruvu Girls High School Box 72, MLANDIZI To the Medical Officer, ………………………………………………., ………………………………………………, …………………………………………., …………………………………. ………………………………………………………………………….(Name in full) Please examine the above named student as to her physical and mental fitness for a full time student. The examination should include the following categories (a-d). a. (i) Eyesight (ii) Hearing (iii) speech (iv) limbs (v) general diseases (vi) leprosy (vii) epilepsy. b. Neurosis c. Other serious diseases e.g. Asthma, T.B etc. d. Pregnancy Name……………………………………………………date……………………………signature…………… PART B: MEDICAL CERTIFICATE i) Eyesight…………………………………………… ii) Hearing……………………………………………. iii) Speech……………………………………………. iv) General disease…………………………………… v) Leprosy…………………………………………… vi) Epilepsy…………………………………………… vii) Neurosis…………………………………………. viii) Other serious diseases e.g. asthma………………. ix) T.B……………………………………………………. x) Pregnancy Comment…………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………. Name……………………………………….date…………………………….signature……………. STATION……………………………………………….DESIGNATION…………………………. HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA
SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA RUVU, S.L.P. 72, MLANDIZI
AHADI YA KUKUBALI KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI RUVU
1. Jina la mwanafunzi……………………………………………………………………………. 2. Jina la kijiji au mtaa atakako…………………………………………………………………. 3. Jinan a anuani ya mzazi/mlezi na namba ya simu……………………………………………………………………………………………. …………………………………………………………………………………………………. 4. Mimi (jina la mwanafunzi)…………………………………………………………………… Nimekubali kujiunga na shulle ya sekondari Ruvu. Wakati wote naahidi kuwa m tiifu kufuata na kuzingatia taratibu za shule, kutunza mali y a umma na kufanya kazi kadri ya uwezo wangu na juhudi na maarifa. 5. Nafahamu kwamba kitendo chochote kilicho kinyume na mwenendo na utaratibu wa shule kinastahili adhabu kali hata kama itakavyoamuriwa na jumuiya ya shule pamoja na bodi ya shule. 6. Nimeyaona maagizo yote nimeyasoma na kuyaelewa. i) Sahihi ya mwanafunzi…………………………………………………………………………. ii) Sahihi ya Mzazi/Mlezi…………………………………………………………………………. iii) Tarehe…………………………………………………………………………………………. 7. Barua zote zinazohusu mahitaji ya shule narippoti za shule ziende kwa anuani ya Mzazi/Mlezi……………………………………………………………………………………………. WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
MAAGIZO MUHIMU YA VITABU VYA KIADA NA ZIADA

Ili mwanafunzi aweze kupata elimu bora na yenye kumwezesha kukabiliana na mazingira halisi, anapaswa kuwa na
vbitabu, Hapa ni baadhi ya vitabu ambavyo anapaswa kuja navyo ili aweze kumudu sawa sawa mchepuo wake.
1. HISTORY
Nyirenda H.D (1991) Africa in world History, Dar es salaam, Dup. Ltd Nyireda H.D (1992) topics in African history Dar es salaam dup. Ltd Water R. (1973) how Europe under developed Africa, Dar es salaam DUP 2. SCIENCE AND PRACTICE OF AGRICULTURE
Envents G.W (1967) East african weeds and their control their control Morgan,C.A. et at animal nutrition addision Wesley Longman United Kingdom URT management of important crop pests and diseases in Tanzania ministry of agriculture and food security Urio, PC introductory to soil science Tanzania publishing House Dare s salaam. 1. H.Gora Kimbunga (taasisi ya uchunguzi wa Kiswahili (YUKI) 2. Shabani Robert Mapenzi boara Robert (Mkuki na nyota) 3. T.A Mvungi Chungu Tamu (Tanzania publishing) 4. M.S. Khatibu Fungate ya Uhuru (macmillan and Aidan) 1. Shaban Robert (2003) kufikirika (mkuki na nyota) 2. Shafi A. (1999) vuta ni kuvute, Mkuki na Nyota 3. Tuwa, H (2007) mfadhili, melthew B/S and stationery 4. Mbunda, S (2007) Usiku utakapokwisha – Mackmilian and Aidan.
TAMTHILIYA

1. Mbogo E. morani –(DUP) 2. Mohamed S. Kivuli kinaishi (Oxford University pres) 3. E. Hussein kwenye ukingo wa thim (Oxford university press 1) 4. Nguzo mama (UDP) ENGLISH

1. Mloko POETRY (2002) The wonderful surgeon and other poems, mkuki na nyota
2. Tanzania Insitute of education (1996) selected poems, pint park (T) Limited

NOVEL SHORT STORESIS

1 Armah A. (1996) the beautiful ones are not y et born, E.A.E.P
Achebe C, (1991) A man of the people. E.A.E.P
Danny (1983) His excellence the head of state, MacMillan Aidan
i) Lubuga F, (1990) Betrayal in the city, Heinemann ii) Nyugi wa thiongo et at (1982) I will marry when I want iii) Ibsemn H (1974) An enemy of the people, Etre metheuman
GENERAL STUDIES

i) Mganywa B.M general studies for advanced level ii) Nyangwine, A Note for generals studies form five and six iii) Abmadiyya – communication skills, theory and practice.
GEOGRAPHY

i) Mock H, principle of physical geography ii) Bunnet, general geography and diagram iii) Stanler, introduction to physical geography i) Nelkon and parker, principle physics ii) Roger, M – physics iii) Kiiza, R solved major problems in physics i) Michael R. Advanced biology for secondary schools ii) Taylor O.J stoud G.W bilogicalscience iii) Msaky, L. cell structure of organization iv) Understanding biology CHEMISTRY

i)

ADVANCE MATHEMATICS
Chandi, S – mathematics statistics and probability ELIMU NI UKOMBOZI
MKUU WA SHULE

Source: http://ruvugirlshighschool.sc.tz/userfiles/MAAGIZO_YA_KUJIUNGA_NA_SHULE.pdf

agfax.net

Using DDT for indoor mosquito control Amadou Sowe - Manager, Health Education Programme, The Gambia Summary The chemical DDT has been banned for use as an agricultural pesticide under an international agreement, the Stockholm Convention, as DDT can have long term impacts on the environment. However, use of DDT to kil malaria‐carrying mosquitoes is stil allowed, and in The Gambia

obhok.net

Schizophrenia What is schizophrenia? Schizophrenia is a chronic, severe, and disabling brain disorder that has affected people throughout history. About 1 percent of Americans have this illness.1 People with the disorder may hear voices other people don't hear. They may believe other people are reading their minds, controlling their thoughts, or plotting to harm them. This can terrify peo

Copyright © 2010 Medicament Inoculation Pdf